TAARIFA
YA UTENDAJI KAZI KATIKA SERIKALI YA WANACHUO (ARISO) MWAKA 2016/2017
Tunapenda kumshukuru
Mungu wetu kwa wema na ulinzi wake tangu tulipokabidhiwa uongozi hadi leo tuko
salaama, jina lake litukuzwe sana.
Tulikabidhiwa uongizi rasmi tarehe 15/06/2016
na tukiwa jumla ya wanachuo 171
Malengo na madhumuni ya taarifa hii ni kujua mafanikio,malengo na changamoto katika serikali yetu ya ariso.
Chama cha ariso
kilikuwa na malengo mbalimbali kama yalivyokuwa yanapendekezwa kwenye vikao na
kwa kujinadi kipindi tunaomba kura kwenu kama ifuatavyo;
MALENGO
I.
Kuinua uchumi wa ariso kwa kubuni miradi
mbalimali.kama vile kuwa na jiko la kuchoma chipsi , kuwa na photocopy mashine
kuwa na mashine ya kutengeneza vitambulisho itakayo kuwa ikitengeneza
vitamburisho na vyeti katika chuo chetu na katika vyuo mbalimali na tasisi
mbalimbali itakayo kuwa kama kitega uchumi wa ariso.
II.
Kutengenza brogspot itakayo tumiwa na wanachuo na watu mbalimbali kupata
tarifa za chuo.
III.
Kununua computer itakayotunza kumbukumbu
za ariso kwa kila mwaka
IV.
Kusimamia matatizo yote ya wanachuo na
kuhakikisha kila mwanachuo ameyafikia malengo yake kwa dhati .
V.
Kusimamia ratiba ya masomo kuhakikisha
kila darasa lina pata siku moja kwa kila wiki kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
VI.
Kusimamia swala la maji, chakula pamojan
na mazingira kwa ujumla
VII.
Kusimamia pesa na mali za ariso
MAFANIKIO;
Mafanikio
yaliyopatikana tangu tupewe uongozi ni mengi , kwa kuyataja kwa ufupi tu.
I.
Tumefanikiwa kusimamia matatizo na kero nyingi zinazotukabiri
wanachuo kama vile ukosefu wan ndoo, mifagio ya vyumbani taa katika mabweni,
taa madarasani, ubovu wa ofisi ya ARISO na mbao za kufundishia na kero
zinginezo nyingi.
II.
Tumefanikiwa kufungua blonspot inayoitwa arisoardhi.blogspot
ambayo ina email. Ariso.ardhi@gmai.com
hii itatusaidia wanachuo kupata habari
mbali mabali katiaka chuo chetu.
III.
Tumefanikiwa kupeleka namba za simu za
wanachuo na kusajiliwa na vifurushi vya university offer tigo na voda
IV.
Tumefanikiwa kusimamia swala la ratiba
na kuhakikisha kila darasa limepata siku moja kwa kila wiki kwa ajili ya
mafunzo kwa vitendo.
V.
Tumefanikiwa kuanzisha mafunzo ya
programs zinazoendana na masomo yetu tuliyoyaedesha kwa ratiba za usiku hii imesaidia kujua program vizuri kwa kila
mwanachuo kama vile Autocard na Arc GIS.
VI.
Tumefanikiwa kupewa week moja kwa ajili
ya kujifunza practical kwa vifaa vya kisasa ikiwa kama study tua kwa wanafunzi.
VII.
Tumefanikiwa kusimamia swala la maji kwa
kuhakikisha maji yanapatikana kwa kila mda na kuomba kuongezewa kwa tank za
maji hapa chuoni.
VIII.
Tumefanikiwa kusimamia pesa ya ariso kwa
kuhakikisha tumepewa kama pesa ya wanachuo
IX.
Tumefanikiwa na kusajiliwa kwa account
yetu ya ARISO na BOT
X.
Tumefanikiwa kufanya sherehe ya
kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa kwanza.
XI.
Tumefanikiwa kusimamia DSTV na kuomba
chuo watulipie kifurushi cha DSTV .
XII.
Tumefanikiwa kushirikiana na vyuo
vingine katika sherehe mbalimbali kimawazo pamoja na michezo.
XIII.
Tumefanikiwa kununu vifaa vya michezo
kama vile mipira
XIV.
Tumefanikiwa kupewa mipira miwili na
watu wa LAPF na tumeomba jezi pia bado tunasubilia .
XV.
Pia tumefanikiwa kujumuika na watu wa
tigo wakatupa huduma zao na pia tukafanikiwa kuwaomba watuwezeshe vifaa vya
michezo kama vile jezi pamoja na mipira
na pia wakakubari kuwashirikisha katika sherehe zozote pale tunapoandaa sherehe
zetu kama vile welcome first year na graduation .
CHANGAMOTO
Zifutazo ni changamoto
zilizo tukabiri katika utendaji kazi
I.
Ukosefu wa mtaji utakao tuwezesha
kuendesha miradi mbalimbali itakayo kuwa
kama kitega uchumi wa ariso.
II.
Kutotekelezewa kero zetu mapema pale
tunapo pata changamoto hapa chuoni .
III.
Ukosefu wa viwanja vya michezo hili
limekuwa likitupa wakati mgumu sana pindi tunapohitaji mazoezi
IV.
Kutokuwa na bima kwa baadhi ya wanachuo
hii imekuwa ikitupa wakati mgumu pale mwanachuo anapopatwa na tatizo kama vile
kuumwa hadi inapelekea kwa viongozi kutumia pesa zao kutoka mifukoni mwao
kumsaidia mwanachuo.
MAPENDEKEZO
· Tunapendekeza
uongozi utakao kuja uhakikishe kusimamia
kero bila kurudi nyuma
· Mapendekezo
yetu kuwa kwa wanachuo wote ambao hawana bima za afya ni ushauri kuwa kila
mwanachuo awe na bima ya afya hii itamsaidia pale anapokuwa na tatizo lolote la
kiafya .
· Uongozi
ujao usimamie swala la practical kwa kila darasa lipate hata siku moja kwa
week.
· Pia
tunapendekeza viongozi watakaochaguliwa wasimamie kujifunza kwa programs na
kuhakikisha kila mwanachuo anajua hizo software.
HITIMISHO
Shukrani
za pekee kwa wanachama wote wa ariso kwa
ushirikiano wenu katika uongozi wetu muendele na moyo wa kusaidiana ili kuanda
maisha yetu kwa pamoja na kuijenga ariso.
kwa
niaba ya viongozi wenzangu tunasema asanteni sana Mungu awe pamoja nanyi
awaongoze katika maandalizi ya mitihani na katika mitihani yetu.
0 comments :
Post a Comment