WIZARA YA ARDHI NYUMBA
NA MAENDELEO YA MAKAZI CHUO CHA ARDHI MOROROGO
RISALA YA WANAFUNZI WA
CHUO CHA ARDHI MOROGORO KWA MGENI
RASMI MAHAFALI YA 35 YA CHUO CHA ARDHI
TAR 24/03/2017
Ndugu mgeni rasimi,
Awali
ya yote tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kufika kwako hapa chuoni
,tunatambua kuwa umeacha shughuli zako nyingi za kiofisi na ukakubali kuchukua
muda wako kuja kujumuika nasi katika shughuli ya kuwaanga ndugu zetu kwa pamoja
tunasema asante sana Mungu awe pamoja nawe na karibu sana.
Ndugu mgeni rasimi;
Chuo
hiki kiko chini ya wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi na kilisajiliwa na Baraza la Taifa la elimu ya ufundi
Tanzania (NACTE) tangu tarehe 21/5/2002
na chuo kinatumia mitaala ambayo ni
“Competence based “ chuo kilipata ithibati
kamili (Full Accreditation) ya NACTE tangu mwaka 2010. Baada ya kutimiza vigezo
vya elimu na mazingira ya uboreshaji elimu hiyo.
LENGO
LA RISALA:
Ndugu
Mgeni Rasmi,
Lengo la risala hii ni kukujulisha
kuhusu mafanikio, changamoto, maoni na mapendekezo katika kuboresha hali ya
kitaaluma na maisha mengine nje ya taaluma Chuoni hapa.
Ndugu mgeni rasimi; Chuo
kinatoa kozi ya Jiomatikia katika ngazi zifuatazo:
Cheti
cha awali cha Jiomatikia (Basic Certificate in Geomatics (NTA LEVEL 04)),
Astashahada
ya Jiomatikia (Certificate in Geomatics (NTA LEVEL 05)),
Stashahada
ya Jiomatikia (Diploma in Geomatics (NTA LEVEL 06)).
Ndugu mgeni rasimi:
Katika
mahafali ya leo, kuna jumla ya wahitimu 171 kati yao wanafunzi wa jinsia ya
kiume wakiwa ni 136 Na jinsia ya kike wakiwa
ni 35.
Ndugu mgeni rasimi;
Mafanikio
yaliyopatikana tangu chuo chetu kianzishwe ni mengi , kwa kuyataja kwa ufupi tu
ni kwamba kila mwaka chuo kimekuwa kikizalisha wataalamu wazuri wenye kuleta ufanisi
katika taaluma hii ya upimaji Aridhi, nchini ambao wameajiriwa katika Halmashauri
mbalimbali na hivyo kuipunguzia serikali utegemezi wa wataalamu wa kigeni
katika idara ya upimaji Ardhi.
CHANGAMOTO
Ndugu mgeni rasimi:
Malengo
ya serikali ni utekelezaji wa sera ya upimaji ardhi kwa ajili ya mashirika na
taasisi mbalimali, kutokana na ukosefu wa ajira wataalamu wengi hawanufaiki na
taaluma inayotolewa katika chuo hiki hadi kupelekea wengi wetu kupoteza taaluma
zetu kwa kukaa tu bila ajira. ndugu mgeni rasimi:
kutokana na tatizo la ajira tunaamni wizara
yako inao uwezo wa kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hili kwa kutoa ajira pindi
tunapomaliza muda wa mafunzo.
Ndugu mgeni rasimi:
Tunalo
tatizo katika chuo chetu la kukosa vitendea kazi kwa ajili ya masomo yetu; Tunao Ukosefu wa maktaba (Library) kwani
iliyopo bado haijaisha, jengo hili la maktaba limekuwa na muda mrefu tangu
lifikie hatua hiyo, kwa sasa tuna chumba
kidogo cha kutunzia vitabu hivyo hali hii inatupa wakati mgumu wa kujisomea
kwani tunakosa vitabu vya kutosha.
Ndugu mgeni rasimi;
Tunao Ukosefu wa chumba
cha computer (Computer Lab) kwani kilichopo ni kidogo chenye computer chache na
baadhi ni mbovu hazitumiki, pia computer hizi hazina program za kitaaluma (software).
Ndugu mgeni rasimi;
Tunao
Upungufu wa vifaa vya kujifunzia vinavyo endana na taaluma yetu kwani vilivyopo
ni vichache, na vingine vimeshapitwa na wakati tunaomba tupatiwe vifaa za
kisasa kama vile RTK GPS, na Differential GPS za kutosha ili tupate elimu
inayoendana na wakati.
Ndugu mgeni rasimi;
Tunao
Ukosefu wa vibweta vya kujisomea kwenye mazingira ya chuo, hivyo wanachuo
kufanya majadiliano ya kimasomo (Group Discussion) kwenye mazingira magumu,
Ndugu mgeni rasimi;
Serikali
kupitia wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi ilikuwa ikitupatia stationary Allowance Tsh 50,000 /= kila
mwanachuo, pesa hii ilikuwa inasaidia
kumudu gharama zote za stationary kwa wanachuo lakini mwaka wa masomo 2016/2017
hatujapewa hii imepelekea kwa mwanchuo kuto mudu gharama za stationary.
Ndugu mgeni Rasimi;
ombi letu kuwa serikari kupitia wizara ya Ardhi
Nyuma na Maendeleo ya makazi ituhudumie stationary allowance kwa kila
mwanafunzi kwa kila mwaka kama ilivyokuwa hapo awali, pia tunaomba mchakato wa
kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati uharakishe ili kupunguza ugumu wa
kugharamia elimu wazazi wetu.
Ndugu mgeni rasim;
Miundombinu
mingi imechakaa na ina tufanya tuishi katika mazingra magumu; Uchakavu wa
madarasa (madirisha, feni na mifumo ya umeme kusababisha hitilafu kila mara
madarasani). Mabweni yaliyopo yamechakaa sana, sakafu, paa, kuta, madirisha, na
milango vimechakaa sana kiasi cha kutokuwa rafiki kwa wanachuo na hayatoshi.
Hivyo kupelekea kukaa wanafunzi wastani wa sita mpaka nane chumba kimoja. Uchakavu
wa vyoo vyote vinavyo patikana hapa chuoni kwani vingi havijafanyiwa ukarabati
vinaziba mara kwa mara na kusabisha usumbufu kwa wanachuo.
Ndugu mgeni rasimi;
Chuo
hakina viwanja vya michezo, hii inatupa wakati mgumu tunapohitaji mazoezi
nakupelekea kushindwa kuendesha michezo hapa
chuoni. Tunaomba uwezeshwaji kutoka wizara yako wa kujenga eneo la chuo
lililopo mlima kola. Tunao upungufu wa tank za kutunzia maji, hii imepelekea
kutokuwa na uhakika wa maji hapa chuoni kwani tank iliyopo ni ndogo na
halikidhi mahitaji.
Ndugu mgeni rasimi;
tunakutakia
kila la kheri katika kazi zako za ujenzi wa Taifa na tunatumaini na kuamini
kuwa matatatizo tuliyowasilisha kwako katika risala hii yatapatiwa
ufumbuzi wa kudumu. Nasi kwa pamoja tunashukuru sana kwa kuweza kuonesha moyo
wa upendo, kujali na kuvumilia yote na kuweza kufika hapa chuoni isiwe kikomo
chako cha kututembelea mara kwa mara kujua maendeleo ya chuo chetu na mapungufu
yatakayojitokeza katika chuo chetu tukiwa kama wanafamilia wa wizara yako Mungu
awe pamoja nawe .
Risala
hii imeandaliwa na Mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Ardhi
Morogoro
NDG.
MAGOMBA PETER MAHOTA- RAIS ARISO
………….Ahsante sana…………..
0 comments :
Post a Comment