Hata hivyo, tafiti nyingi duniani zinaonyesha kwamba kila mtu anakipaji chake na anaweza kufanya vizuri zaidi kwenye kazi fulani kuliko kazi nyingine. Kwetu sisi hapa Tanzania, mtu anaposoma kozi yoyoye tu ilimradi amalize chuo, ni dhahiri kwamba japokuwa kijana huyo atamaliza chuo lakini atakuwa ameua au amefifisha kwa kiasi kikubwa kipaji chake. Mpaka aje kurejea tena kwenye mstari inakuwa ngumu sana wakati mwangine anashindwa kabisa.
Vijana wanaojiunga chuo naweza kuwaweka katika makundi matatu, kulingana na namna wanavyo chagua kozi za kusoma chuoni. Makundi hayo nimeyapata baada ya kufanya mazungumzo na vijana wengi wanaojiunga chuo, waliopo chuoni na hata waliomaliza chuo. Kwa niaba yao watawakilishwa na hawa watatu, Jackline, Dorine na binti yake Mwalimu Christopher Mwakasege.
Kundi La Kwanza: Linawakilishwa Na Jackline
Jackline ni rafiki yangu kwa sasa anasoma kidato cha nne. tarehe 22/08/2015 nilifanya nae mahojiano nikamwuliza; Jackline, utakapomaliza kidato cha nne na kuendelea na masomo ya chuo ungependa uchukue kozi gani?. Akajibu akasema mimi kozi yoyote tu nitakayochaguliwa. Nikamwuliza tena kozi yoyote? Kwani moyoni mwako unapenda uwe nani? Akasema, “mimi kazi yoyote tu nikatayopata”.
Kutokana na majibu ya Jackline, anawakilisha kudi kubwa la vijana wanaomaliza masomo yao ya kidato cha nne au kidato cha sita halafu hawajijui wanapenda wawe akina nani, na kwa sababu hiyo, kozi yoyote wako tayari kusoma ilimradi wamechaguliwa kwenda chuo. Kundi hili sio zuri sana kwa sababu wewe kama kijana unatakiwa ujichunguze mapema na ujiandae kusomea kile unachokipenda vinginevyo utapeperushwa kama bendera.
Sifa moja kubwa ya kijana aliyeko kundi hili hataumia wala kuhuzunika pale anapochaguliwa kozi yoyote, kwake yote ni sawa. Lakini Brian Tracy katika kitabu chake “The Goal” anatushauri kuwa na malengo katika maisha yetu ili tuweze kufikia mafanikio makubwa. Anasema hivi “Viongozi wakubwa na matajiri wengi wanajitambua wao ni akina nani, na kwahiyo, kila siku hufuata maono yao, lakini watu wengi masikini nawa daraja la kati hawajitambui wala hawana maono au kama wanayo wanavurugwa na kwa sababu hiyo hawafuati ndoto zao na kufanikiwa kwao ni kugumu sana”.
Kundi La Pili: Linawakilishwa Na Dorine.
Dorine anatarajiwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma mwaka huu maana ameshachaguliwa tayari. Nilifanya naye mahojiano siku chache zilizopita nikamwuliza Dorine, “Umechaguliwa kujiunga na chuo ,vipi unaridhika na kozi uliyochaguliwa? Akasema, “akah”! Mimi hata sipendi”, Nikamwuliza hupendi?, Sasa utafanyaje umeshachaguliwa tayari?, Akasema “Mimi ngoja niende tu nikasome ila nikimaliza nabadilisha kozi, maana kozi hii siipendi kabisa”.
Kutokana na majibu ya Dorini, anawakilisha kundi kubwa la vijana wanaojiunga chuo kwa masomo au kozi wasiozipenda, lakini inawalazimu tu kwenda kusoma kwa sababu asipoenda inakuwa shida. Kijana aliyeko kwenye kudi hili ni yule anayejitambua na anatamani siku moja afikie ndoto zake lakini mfumo wa elimu unajaribu kuua au kufifisha kabisa ndoto zake.
Pamoja na hayo, maadamu kijana aliyeko kwenye kundi hili, anajifahamu yeye ni nani, kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kubadili maisha yake na akafanikiwa ngawaje inaweza kuwa ni kwa kuchelewa.
Kundi La Tatu: Linawakilishwa Na Mtoto Wake Mwalimu Christopher Mwakasege.
Tarehe 26/08/2015, Mwalimu Christopher Mwakasege akiwa katika uwanja vya Furahisha, Mwanza, alielezea kisa cha binti yake mwenye msimamo. Alisema amekuwa akiwafundisha watoto wake kujiamini na kukifuata kila kinachoitwa ndoto au matamanio yao. Sasa, kisa kikaja kwa binti yake ambaye baada ya kumaliza kidato cha sita alitaka kusomea urubani. Anasema, alijitahidi kumtafutia chuo kinachotoa mafunzo ya urubani lakini kwa muda mrefu hakufanikiwa, basi akamshawishi binti yake alegeze msimamo aende chuo kingine chochote. Binti alikubali kwa shingo upande akaenda chuo kimoja kiko Afrika Kusini lakini alisoma kwa wiki moja tu akapigia simu baba yake kumwambia masomo yamemshinda. Ilibidi arudi nyumbani na baadaye sana walifanikiwa kupata chuo cha urubani akaenda huko na sasa ni rubani.
Mfano huu wa huyu binti, anawakilisha vijana wengi wenye misimamo wanaojua karama zao na huwa wako makini kuhakikisha wanapata nafasi ya kusoma kozi wanayoitaka, hawa mara nyingi hufanikiwa sana katika maisha yao.
Kutokana na makundi haya matatu tunajifunza kwamba, mfumo wa elimu unaweza kukuvuruga na kukutoa kwenye laini yako unayotaka na matokeo yake unaweza ukasoma kozi ambayo huipendi, hata kama utakuja kuajiriwa kwa kozi hiyo utafanya kazi chini ya kiwango kwa sababu huipendi kazi hiyo. Kwa lugha nyingine unakuwa umechagua huzuni ya siku nyingi na ukisoma kozi unayoipenda unakuwa umechagua furaha.
Ukigundua kuwa unasoma au umesoma kozi inayokupa huzuni unafanyaje?
Jibu ni rahisi tu “Unatakiwa kuchepuka mapema”.
Kuchepuka ndo nini?. Kuchepuka kwa lugha rahisi ni kuachana na kozi hiyo kabisa na ukajibidiisha kupata kitu unachokitaka.
Kuna njia mbili za kuchepuka mapema
Njia ya kwanza: Rudi Chuo Tena Ukasome Kile Unachokitaka.
Kwa hili nakupa mfanyo wa Tajiri namba moja Tanzania Mohamed Dewji, yeye alipoona kozi aliyochukua haitamsaidia na haipendi aliamua kurudi chuoni tena kusomea masomo yale anayotaka. Sasa hivi, kutokana na ubunifu wake huo ameweza kuwa tajiri wa kwanza Afrika mashariki huku akiwa nafasi ya 24 ya matajiri wakubwa Barani Afrika.
Njia ya pili: Jifunze Mitaani
Kufahamu namna ya kujifunza mtaani soma makala hii
Mwandishi mashuhuri wa vitabu na tajiri, Robert Kiyosaki anasema “Njia rahisi ya kukufanya ufanikiwe mapema na utajirike mapema ni kupata elimu, na hasa elimu ya fedha, na njia rahisi ya kukupa elimu hiyo ni kusoma vitabu na kushiriki semina nyingi kadri uwezavyo”. Mimi, kwa mfano, sijasomea chuo chochote nikiwa na kozi ya IT, lakini nikiwa mtaani nimejifunza mambo mengi sana yanayohusiana na kozi ya IT. Kama mimi nimeweza ninaimani na wewe utaweza, ingawaje kuna baadhi ya kozi huwezi ukajifunza mtaani mfano udaktari, basi kama ni hivyo rudi chuoni mapema ili uweze kuifikia ndoto yako.
“Mtu anaposoma kozi yoyoye tu ilimradi amalize chuo, ni dhahiri kwamba japokuwa kijana huyo atamaliza chuo lakini atakuwa ameua au amefifisha kwa kiasi kikubwa kipaji chake. Mpaka aje kurejea tena kwenye mstari inakuwa ngumu sana wakati mwangine anashindwa kabisa”
Tutembelee kwenye
www.morningtanzania.com
0 comments :
Post a Comment