Maana ya maisha
kila siku nashindwa kupata majibu ya maswali ya fuatoyo je na wewe ?
- Maana ya maisha ni nini?
- Nini maana ya haya yote?
- Sisi ni nani?
- Kwa nini tumekuwepo?
- Sababu ya sisi kuwa hapa ni nini?
- Asili ya uhai ni nini?
- Hali ya maisha ni nini?
- Ukweli ni nini Madhumuni ya maisha ya mtu ni nini?
- Cha maana na cha thamani maishani ni nini?
- Thamani ya maisha ni nini
- Sababu ya kuishi ni nini?
- Kwa nini tunaishi
Maana ya
maisha ni mojawapo kati ya masuala kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa
binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza
katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha
yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?
Binadamu
anajiuliza maswali kama hayo hasa anapokabiliana na kifo, kwa mfano msiba wa
ndugu au rafiki.
Limekuwa
suala kuu la udadisi kwa sayansi, falsafa na teolojia tangu zamani. Kumekuwa na
idadi kubwa ya majibu kwa maswali hayo kutoka asili mbalimbali kiitikadi na
kiutamaduni.
Maana ya
maisha imechanganyikana kwa undani na dhana za falsafa na imani za dini na
hugusia masuala mengine mengi, kama vile ontolojia, tunu, kusudi, maadili,
hiari, uwepo wa Mungu, roho, na kinachoendelea baada ya maisha haya.
Michango ya
sayansi kawaida ni ya moja kwa moja na inaeleza uhalisia kutokana na mambo
yanayopimika kuhusu ulimwengu; sayansi inatoa muktadha na mipaka kwa mazungumzo
kuhusu mada zinazohusika.
Mbadala ni
mtazamo wa kifalsafa unaokabili
swali: "Ni nini maana ya maisha 'yangu'?" Thamani ya swali linalohusu
kusudi la maisha huweza kuwiana na kuupata ukweli wa mwisho, au hisia za umoja,
au hisia ya utakatifu.
Maswali na marejeo yake
Mwanafalsafa
katika kutafakari alivyochorwa na msanii Rembrandt.
Maswali
kuhusu maana ya maisha yameulizwa kwa njia mbalimbali zenye upana, yakiwemo
yafuatayo:
Uchunguzi wa kisayansi
DNA ambayo
ina maelekezo ya kijenitikia kwa ajili ya maendeleo na utendaji wa viumbe hai
vyote.
Kwamba
sayansi inaweza kutusaidia kuelewa zaidi kuhusu masuala ya msingi (kama vile
maana ya maisha) ni suala linalozua mabishano mengi katika jamii za sayansi na falsafa ya sayansi.
Hata hivyo,
sayansi inaweza kutupa muktadha fulani na huiweka baadhi ya mipaka ya
mazungumzo kuhusu mada kama hizo.
Umuhimu wa kisaikolojia na thamani katika maisha
Sayansi
huenda ikashindwa kutuambia nini ni cha thamani maishani, lakini baadhi ya fani
zake hugusia maswali yanayohusiana: watafiti katika saikolojia chanya hutafuta
sababu zinazoleta hali ya ndani ya kuridhika na maisha.kujihusisha vikamilifu
katika shughuli, kufanya mchango zaidi kwa kutumia vipawa vya kibinafsi,
Aina moja ya
mfumo wa thamani iliyopendekezwa na wataalamu wa elimunafsia ya jamii, iitwayo
kwa upana "Nadharia ya Kupambana na Mambo ya Kutisha", inasema kwamba
maana yote ya binadamu inatokana na hofu ya msingi ya kifo, ambapo maadili
yanachaguliwa yanapotusaidia kuepukana na kumbukumbu ya kifo.
Sayansi ya
niurolojia imetunga nadharia ya malipo, raha na msukumo katika masuala ya
kimwili kama shughuli za kupitisha ujumbe za kiniuro. Ikiwa mtu anaamini kwamba
maana ya maisha ni kufanya raha ziwe nyingi iwezekanavyo, basi nadharia zinatoa
utabiri unaozidi kuongezeka, kuhusu jinsi ya kufanya ili kufanikisha hilo.
Somo la
kijamii linapima thamani katika ngazi ya kijamii kwa kubuni nadharia kama vile
nadharia ya thamani kanuni, anomi, n.k.
Asili na
hali ya maisha ya kibiolojia
Kufanya kazi
kwa abayojenesisi hakueleweki kwa ufasaha: nadharia mashuhuri ni pamoja na
nadharia ya dunia ya RNA (vitoaji aina sawa katika makao ya RNA) na nadharia ya
dunia ya chuma-sulfuri (umetaboli bila Jenetikia). Nadharia ya mabadiliko ya
viumbe haijaribu kuelezea asili ya uhai, bali mchakato ambao viumbe tofauti
vimepitia katika kipindi chote cha historia kupitia mabadiliko ya ghafla ya
kijenitikia na uteuzi wa kiasili Wakati
wa mwisho wa karne ya 20, kwa kuzingatia ufahamu wa mabadiliko ya viumbe unaotegemea
jeni hasa, wanabiolojia George C. Williams, Richard Dawkins, David Haig,
miongoni mwa wengine, wanahitimisha kwamba ikiwa kuna kazi msingi ya maisha, ni
kujinakilisha kwa DNA na kuendelea kuwa hai kwa jeni za mtu.
Ingawa
wanasayansi wameyachunguza maisha yalivyo duniani, kuyafafanua bayana bado ni
changamoto. Kimwili, mtu anaweza kusema
maisha "hula entirofi hasi" ambayo walio hai wanapunguza entirofi yao ya
ndani kwa gharama ya aina fulani ya nishati inayochukuliwa ndani kutoka
mazingira.
Wanabiolojia
kwa jumla wanakubaliana kwamba viumbe mbalimbali ni mifumo inayojipanga
inayosimamia mazingira ya ndani ili kudumisha hali hii ya mpango, shughuli za
kimetaboliki hutumika kutoa nishati, na uzazi unaruhusu uhai kuendelea kwa
vizazi vingi. Kwa kawaida, maumbile huwa sikivu kwa uchochezi na habari za
kijenitikia, hivyo huelekea kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi ili kuruhusu
marekebisho kupitia mabadiliko ya kimwili. Sifa hizo huongeza nafasi ya kuishi
ya kiumbe binafsi na wazao wake kwa mtiririko huo.
Viwakala
visivyokuwa vya seli vinavyozaana, hasa virusi, kwa jumla havitazamwi kama
viumbe kwa sababu haviwezi kuzaana kwa "kujitegemea" au kuendesha
shughuli za kimetaboliki. Pambano hilo ni tatizo, ingawa baadhi ya vimelea na
visimbayonti vya ndani ya mwili pia vinaweza kuishi maisha ya kujitegemea.
Astrobiolojia
inajihusisha na masomo ya uwezekano wa kuwa na aina tofauti ya viumbe hai
katika ulimwengu mwingine, kama vile miundo ya kujinakilisha kutoka vifaa
vingine visivyo DNA.
Asili na hatima ya ulimwengu
Upanuzi wa
kimetriki wa nafasi. Enzi ya kupanda ni kupanuka kwa kivuto cha kimetriki
kilichoko upande wa kushoto.
Ingawa dhana
ya Mlipuko mkuu ilipozinduliwa mara ya kwanza ilipambana na shaka kwa wingi,
shaka iliyochangiwa na uhusiano na imani ya dini ya uumbaji, imekuja kuungwa
mkono na uchunguzi kadhaa wa kujitegemea.] Hata hivyo, fizikia ya sasa inaweza
kuelezea tu ulimwengu ulivyokuwa mapema sekunde 10 baada ya kutokea.
Wanafizikia wengi wamedadisi nini inaweza kuwa imetangulia, na jinsi ulimwengu
ulivyoanza. Baadhi ya wanafizikia hudhani kuwa Mlipuko mkuu ulitokea kiajali,
na kanuni ya kianthropiki inapozingatiwa, mara nyingi hutafsiriwa kuashiria
uwepo wa ulimwengu maridhawa.
Hata hivyo,
haijalishi jinsi ulimwengu ulivyokuja kuwepo, hatima ya binadamu katika
ulimwengu huu ni maangamizi kwani - hata kama ubinadamu utaishi muda huo wote -
maisha ya kibiolojia hatimaye yatashindwa kujiendeleza.
Maswali ya sayansi kuhusu akili
Hali ya
kweli na asili ya fahamu na akili yenyewe pia vinajadiliwa sana katika sayansi.
Suala la hiari pia linaonekana kuwa na umuhimu wa msingi. Masuala hayo
hupatikana zaidi katika nyanja za sayansi koginitivu, niurolojia na falsafa ya
akili, ingawa baadhi ya wanabiolojia wa mabadiliko ya viumbe na wanafizikia wa
kinadharia pia wameliashiria sana suala hilo.
Kuinuka kwa
Watakatifu ni picha iliyochorwa na msanii Hieronymus Bosch. Inaonyesha sehemu
inayofanana na pango lenye mwanga na watu wa kiroho, mara nyingi hutajwa katika
ripoti za waliokikaribia kifo.
Mbinu
nyingine, kwa vile Mfano wa Rasimu Nyingi, hudai kwamba fahamu inaweza kuelezwa
kikamilifu na niurolojia, kupitia utendaji kazi wa ubongo na niuroni zake,
hivyo kushikilia ubiolojia wa kihalisia.
Kwa upande
mwingine, wanasayansi kama Andrei Linde wanadhani kwamba fahamu, kama
nafasi-wakati, huenda ikiwa na ngazi zake za ndani za uhuru, na kwamba maoni ya
mtu binafsi yanaweza kuwa halisi kama (au hata kuliko) vifaa tunavyoweza
kuvigusa na kuviona.
Nadharia
ambazo hazijabainishwa za fahamu na nafasi-wakati zinaelezea kuhusu fahamu
katika kuelezea "nafasi ya vipengele vyenye fahamu", mara nyingi
zikijumuisha idadi kubwa ya mitazamo ya ziada.
Nadharia za
sumakuumeme za fahamu zinatatua tatizo lenye vipengele vingi la fahamu kwa
kusema eneo la sumakuumeme linalotokana na ubongo ndilo hasa linalobeba fahamu
zoefu. Hata hivyo kuna kutokubaliana kuhusu kutekelezwa kwa nadharia kama hiyo
inayohusu utendaji kazi kwingine kwa akili.
Nadharia za akili za kikwontamu hutumia nadharia ya
kwontamu kuelezea baadhi ya sifa za akili.
Ikitegemea
hoja ya maelezo ya akili yasiyoweza kugusika, baadhi ya watu wamependekeza
uwepo wa fahamu ya kikozmiki, wakidai kwamba fahamu kwa kweli ndiyo "msingi
wa yote kuwepo". Wanaounga mkono mtazamo huo wanaelezea
matukio yasiyo vya kawaida, hasa uwezo wa kuhisi usio wa kawaida na uwezo wa
kuyasoma mawazo, kama ushahidi wa uwepo wa fahamu ya juu isiyoeleweka. Katika
matumaini ya kuthibitisha uwepo wa mambo hayo yasiyokuwa ya kawaida,
wanaelimunafsia wa mambo yasiyo ya kawaida wamefanya majaribio mbalimbali.
Uchambuzi unaoangalia mambo yote yaliyopo unaonyesha kuwa idadi ya wenye nguvu
zisizo za kawaida (ingawa ndogo sana) kwa ulinganishaji imebaki thabiti. Ingawa baadhi ya wachambuzi wakosoaji wanahisi kuwa somo la elimunafsia isiyo
ya kawaida ni sayansi, hawaridhishwi na matokeo ya majaribio yake.
Wanaochunguza
mambo haya upya, wanabaki na wasiwasi kwamba matokeo yanayoonekana kuwa na
mafanikio huenda yakawa yanatokana na utaratibu mbaya, na watafiti wasiokuwa na
mafunzo ya kutosha, au mbinu hafifu.
Mitazamo ya kifalsafa
Mitazamo ya
kifalsafa kuhusu maana ya maisha ni itikadi ambazo huelezea kuhusu maisha
kupitia suala la maadili au dhana zinazofafanuliwa na binadamu.
Falsafa za Kale za Kigiriki
Plato na
Aristotle katika Shule ya Athene mchoro wa ukutani wa msanii Raffaello.
Uplato
Plato
alikuwa mmoja wa wanafalsafa wa mwanzo, na mwenye ushawishi mwingi hadi leo - hasa
kwa uhalisia kuhusu uwepo wa viulimwengu. Katika Nadharia ya Maumbo,
viulimwengu havipo kimwili, lakini vipo katika maumbo ya kipepo au kimbingu.
Katika Jamhuri mazungumzo ya mhusika wa mwalimu wake Sokrates yanaelezea Umbo
la Zuri, jambo la kimaadili, hali kamili ya uzuri, hivyo basi kipimo cha ujumla
cha haki. Katika falsafa ya Plato, maana ya maisha ni kufikia umbo la juu zaidi
la elimu, ambalo ni Umbo la Zuri, ambapo mambo yote mema na ya haki yanatoa
umuhimu na thamani. Binadamu wamefungwa na wajibu wa kuyatekeleza mazuri,
lakini hakuna yeyote anayeweza kufanikiwa katika harakati hiyo bila fikira za
kifalsafa, ambazo zinaruhusu elimu ya kweli.
Uaristoteli
Aristotle,
mwanafunzi wa Plato, alikuwa mwanafalsafa mwingine wa mapema, mwenye ushawishi
mkubwa, ambaye alisema kuwa maarifa ya maadili si ya hakika kama metafizikia na
somo la maarifa, lakini ni maarifa ya kiujumla. Kwa sababu si fani ya
kinadharia, inambidi mtu asome na afanye mazoezi ili awe 'mzuri', kwa hiyo mtu
angekuwa mwema, hangeweza kusoma tu fadhila ni nini, ingembidi awe na fadhila,
kupitia juhudi za kiadili. Kufanya hili, Aristotle alifafanua kitendo kilicho
cha fadhila: "Kila tajriba na kila swali, na vilevile kila tendo na chaguo
la tendo, linadhaniwa kuwa na uzuri fulani kama lengo lake. Hii ndiyo sababu ya
kwamba lile zuri limefafanuliwa ifaavyo kama lengo la bidii yote [...]
Kila kitu
hufanywa na lengo, na lengo hilo ni "zuri".
Hata hivyo,
ikiwa kitendo A kinafanyika ili kufikia lengo B, kisha lengo B pia litakuwa na
lengo (lengo C), na lengo C pia litakuwa na lengo, hivyo muundo huo utaendelea
mpaka kitu kiusimamishe. Suluhisho la Aristotle ni Wema mkuu, ambao ni wa
kuwaniwa kwa ajili yake pekee, ni lengo lake lenyewe. Wema mkuu hauwaniwi kwa
ajili ya kufikia mema mengine, na mema yote yanawaniwa kwa ajili yake. Hili
linahusisha kufikia eudemonia, ambayo kwa kawaida hutafsiriwa kama
"furaha", "ustawi", "kutokosa chochote muhimu",
na "ubora".
Falsafa ya Shaka
Katika
Ugiriki ya Kale wanafalsafa wa shaka walisema kuwa lengo la maisha ni kuishi
maisha ya fadhila yanayowiana na viumbe wengine. Furaha inatokana na
kujitegemea na kuusimamia mtazamo wa kiakili; mateso yanatokana na maamuzi ya
uongo kuhusu thamani, ambayo husababisha hisia mbaya na aidha tabia ya uhasama.
Maisha ya
shaka yanakataa tamaa za kawaida za mali, nguvu, afya, na umaarufu, kwa kuwa
huru kutoka vitu vinavyopatikana katika kuyatafuta ya kawaida.Kama
viumbe wenye uwezo wa kufikiria, watu wanaweza kufanikisha furaha kupitia
mafunzo kabambe, kwa kuishi katika njia iliyo ya kiasili kwa binadamu. Dunia ni
ya kila mtu kwa kiwango sawa, hivyo mateso yanasababishwa na uamuzi wa uongo
kuhusu kile ambacho ni cha thamani na kile ambacho hakina maana kulingana na
tamaduni na itikadi za jamii.
Usairini
Falsafa ya
usairini, iliyoanzishwa na Aristipo wa Kirene, ilikuwa shule ya zamani ya
Kisokrate iliyotilia maanani upande mmoja tu wa mafundisho ya Sokrates - kwamba
furaha ni tokeo moja la mwisho la hatua za kimaadili na kwamba radhi ni zuri
kuu; hivyo basi mtazamo wa dunia wa kuipenda raha pekee ambapo kutimiza tamaa
za mwili ni za faida kuliko radhi ya akili. Wasairini walipendelea kutimiza
tamaa haraka kuliko faida inayopatikana baada ya kusubiri kipindi kirefu;
kunyimwa ni huzuni mbaya.
Uepikuro
Mchongo wa
Epikuro akimuegemea mwanafunzi wake Metrodorus katika makavazi ya Louvre.
Kwa Epikuro,
jambo zuri kuliko yote ni kutafuta raha za wastani, kupata utulivu na kuwa
uhuru kutoka hofu (“ataraxia”) kupitia maarifa, urafiki na wema, kuishi kwa
kujichunga; maumivu ya kimwili (“aponia”) hayapo kupitia maarifa ya mtu kuhusu
hali ya dunia na mipaka ya matamanio ya mtu. Vikiwa pamoja, uhuru kutoka
maumivu na uhuru kutoka hofu ndiyo furaha kuu. Kukusifu kwake kufurahia anasa
ambazo hazijapita kiasi kunakaribia dhana ya "kujiepusha" na raha
zote kama vile ngono na anasa:
Tunaposema...
kuwa radhi ndio mwisho na lengo, hatumaanishi raha za upotevu au raha za
kimwili, jinsi tunavyoeleweka na wachache kwa ujinga, ubaguzi au udanganyifu wa
makusudi. Tukisema radhi tunamaanisha kutokuwepo kwa maumivu mwilini na taabu
katika nafsi. Si kwa mfululizo wa ulevi na kuponda raha, si kwa tamaa ya ngono,
wala kufurahia utamu wa samaki, na vyakula vingine vitamu kutoka meza iliyojaa
vinono, ambavyo huzalisha maisha mazuri; ni fikira za kimakini, kutafuta nje ya
misingi ya kila uchaguzi na kuepuka, na kuikataa mitazamo ambayo hufanya shida
kubwa kuichukua nafsi.
Maana ya
Kiepikuro ya maisha inakanusha kutokufa na dhana ya maisha mengine mbali na
haya ya duniani; kuna nafsi, lakini inaweza kufa kama mwili. Hakuna maisha
baada ya kifo, ingawa mtu hatakiwi kuogopa kifo, kwa sababu "Kifo si
chochote kwetu, kwani yale ambao hunywea, ni bila hisia, na kile ambacho hakina
hisia si chochote kwetu."
Falsafa ya Uvumilivu
Falsafa ya
Uvumilivu hufunza kwamba kuishi kulingana na fikira njema ni kuwa katika uwiano
na mpango wa ulimwengu wa Kimungu, unaotokana na mtu kufahamu logos, fikira ya
ulimwengu wote, thamani muhimu inayopatikana kwa wote. Maana ya maisha ni uhuru
kutoka mateso kupitia apatheia (kwa Kigiriki: απαθεια), yaani kuwa na lengo,
kuwa na "uamuzi wazi" si kutofautiana. Mashauri ya moja kwa moja ya
falsafa ya uvumilivu ni fadhila, fikira na sheria ya kimaumbile, zinazojumuisha
kuendeleza kujidhibiti kibinafsi na ujasiri wa kiakili kama njia za kuzishinda
hisia haribifu. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hanuii kuzizima hisia,
bali kuepuka shida za kihisia, kwa kuendeleza uamuzi wazi na utulivu wa ndani
kupitia uzoefu makini wa kimantiki, kutafakari, na kuziweka fikira pamoja.
Msingi wa
kimaadili wa falsafa ya uvumilivu ni kuwa "zuri liko katika hali ya
nafsi", yenyewe inaonyeshwa katika hekima na kujidhibiti, hivyo kuboresha
ustawi wa kiroho: "Fadhila" inatokana na "nia" ambayo
inawiana na maumbile."Kanuni inatumika katika uhusiano wa kibinafsi,
yaani: "kuwa huru kutokana na hasira na wivu".
Falsafa za enzi ya
Kutaalamika
Enzi ya
Kutaalamika na ile ya ukoloni zote mbili zilibadilisha hali ya falsafa ya Ulaya
na kuieneza duniani kote. Ibada na kumnyenyekea Mungu viligeuka kuwa dhana za
haki za binadamu zisizowezwa kunyimwa na dhana ya uwezo wake mkuu wa kifikira.
Maadili ya ulimwengu mzima ya upendo na huruma yaligeuka dhana za kiraia za
uhuru, usawa, na uraia. Maana ya maisha pia yalibadilika, ikiacha kidogo
kuhimiza uhusiano na Mungu na kusisitiza uhusiano kati ya watu binafsi na jamii
yao. Kipindi hicho kilijaa nadharia zinazolinganisha kuwepo kwa maana na
utaratibu wa kijamii.
Uhuru kutoka mipango ya kimali
ya jamii
Uhuru kutoka
mipango ya kimali ya kijamii ni seti ya mawazo yaliyoibuka katika karne za 17
na 18, kwa sababu ya migogoro iliyochukua nafasi kubwa barani Ulaya kati ya
waliozidi kuwa matajiri, pamoja na utaratibu wa viongozi matajiri, na watu wa
dini.
Uhuru kutoka
mipango ya kimali ya kijamii ulionyesha binadamu kama viumbe wenye haki
walizozaliwa nazo na wasizowezwa kunyimwa (pamoja na haki ya mtu kubaki na mali
inayotokana na kazi yake binafsi), na ulitafuta mbinu za kupima haki kuwa sawa katika
jamii yote. Kiujumla, uhuru binafsi ulitazamwa kuwa lengo kuu,[66] kwa sababu
ya kudhani kwamba kupitia hakikisho la uhuru tu haki nyingine zilizojikita kwa
ndani zitakapolindwa.
Kuna aina
nyingi za dhana ya uhuru kutoka mipango ya kimali ya kijamii, lakini dhana zao
kuu kuhusu maana ya maisha zinaambatana na dhana tatu za msingi. Wanafalsafa wa
awali kama vile John Locke, Jean-Jacques Rousseau na Adam Smith waliona
binadamu akianza katika hali ya kimaumbile, kisha akitafuta maana kupitia ajira
na mali, na kutumia mikataba ya kijamii ili kujenga mazingira ambayo yanasaidia
juhudi hizo.
Ukanti
Immanuel
Kant anafahamika kama mmoja wa wanafalsafa wenye ushawishi mwingi zaidi katika
kipindi cha mwisho cha Kutaalamika.
Ukanti ni
falsafa iliyo na msingi katika maandishi ya kimaadili, ya somo la maarifa na ya
kimetafizikia ya Immanuel Kant. Kant anajulikana kwa nadharia ya uwajibikaji
ambapo msingi ni wajibu mmoja wa kimaadili, "dhana ya lazima bila
kujalisha", inayotokana na dhana ya uwajibikaji. Wakanti wanaamini kuwa
vitendo vyote vinafanywa kulingana na lengo au kanuni fulani isiyobainika wazi,
na kuwa ili vitendo vive adilifu, ni lazima viambatane na dhana ya lazima bila
kujalisha.
Kifupi,
mtihani ni kwamba lazima mmoja afanye lengo litumike ulimwenguni kote (tafakari
kwamba watu wote walitenda hivi) kisha angalia kama bado itawezekana
kulitekeleza lengo duniani. Katika kitabu chake, Kazi ya msingi, Kant anatoa
mfano wa mtu ambaye anataka kukopa pesa bila kunuia kuzirudisha. Huu ni utata
kwa sababu kama ingalikuwa hatua ya wote ulimwenguni, hakuna mtu ambaye
angemkopesha mwingine tena kwani yeye angejua kwamba hangerudishiwa pesa hizo.
Lengo la hatua hii, anasema Kant, linaleta matokeo ya mkanganyiko katika
matazamio (na hivyo linapingana na wajibu kamili).
Kant pia
alikanusha kwamba matokeo ya tendo huchangia kwa njia yoyote thamani ya
kimaadili ya tendo, hoja yake ikiwa kwamba ulimwengu wa kimwili upo nje ya
udhibiti kamili wa mtu na hivyo mtu hawezi kuwajibika kwa matukio yanayofanyika
hapo.
Falsafa za karne ya 19
Asili ya
utumikaji inaweza chapwa nyuma sana hadi Epikuro, lakini, kama shule ya mawazo,
inahusishwa na Jeremy Bentham ,ambaye aligundua kuwa asili imemweka mtu
chini ya utawala wa mabwana wawili wa kujitegemea, maumivu na raha. Basi,
kutokana na busara hiyo ya kimaadili, na kuiunda Sheria ya Utumizi, kwamba wema
ni chochote ambacho huleta furaha nyingi zaidi kwa idadi kubwa zaidi ya watu.
Alifafanua maana ya maisha kama "kanuni ya furaha nyingi zaidi".
Bado maelezo yako hayajajibu maswali juu (ya awali)
ReplyDelete