Kabla ya sijaanza kukuletea sababu za wewe kuweka malengo yako kwenye maisha yako naomba nikuulize maswali haya;-
Kwanini ndege hutengeneza viota? Nani huwa anawaambia huu ni wakati wa kutengeneza viota? Tena wanajuaje na wanayapataje material wanayotumia kutengenezea viota vyao?
Ndugu, ndege ni viumbe tunaowazidi akili mara nyingi sana, lakini kinachoshangaza viumbe hawa wanajua majira na nyakati za kuanza kutengeneza viota vyao. Ingawaje material wanayotumia kutengenezea viota hivyo sio rahisi kuyapata lakini ndege hawa husafiri umbali mrefu sana kuyatafuta material mpaka wayapate na siku zote ndege hawa hufanikiwa kuyapata kwa sababu akili na mioyo yao huiamuru kwamba bila kupata material hakuna kutulia. Na kwa sababu kuna msemo usemao; “kila anayetafuta hupata” ndivyo ndege viumbe dhaifu wanavyofanikisha njia zao kwa kutafuta na kupata.
Nikianza kwa kujibu maswali hayo hapo juu. Ndege hutengeneza viota kwa sababu kichwani mwao wana malengo ya kupata watoto. Lakini wanajua ili wapate watoto lazima watage mayai, na ili mayai yasidondoke ovyo wanaamua kutengeneza viota. Kwa hiyo, sababu ya ndege kutengeneza viota sio kutagia mayai bali ni ili wapate watoto. Wanaanza kuangalia kwanza sababu ya wao kutengeneza viota ( mwisho wa malengo) ambayo ni kupata watoto, ndipo wanaanza hatua kwa hatua kwa kufuata picha walioiona ya watoto kutengeneza viota.
Kwa kuwa malengo yao ni kupata watoto, wanaamua kutengeneza mikakati mbali mbali ya kuwapata hao watoto ikiwa ni pamoja na kujenga viota. Pia ili wawapate watoto wanaowataka wanaamua kujifunza majira na nyakati zinazowafaa wao kwa kuwapata hao watoto. Safari ya kupata watoto kwa ndege sio rahisi kwa sababu huwalazimu kusafiri umbali mrefu kutafuta material yanayofaa kwa ajili ya kutagia na hatimaye kupata watoto.
Kwa kifupi ndege hawafanyi yote hayo pasipo malengo. Chakushangaza watu wengi sijui kama wewe ndugu ni miongoni mwao, unataka kupata mafanikio bila kuweka mikakati thabiti itakayokupelekea kufikia hayo matamanio yako yaani hujaweka malengo yako au kama yapo hujayawekea utaratibu kama wafanyavyo ndege wa angani. Mimi nakushauri pata nafasi uwatembelee ndege ukajifunze kwao somo hili.
Sisi MorningTanzania kwa kuliona hilo tunaandaa semina itakayoelezea A-Z jinsi ya kuandaa malengo ya familia yako kuanzia miaka ishirini hadi uzeeni yaani zaidi ya miaka sitini. Kwahiyo unayofursa ya kuipata semina hiyo tutakayoiendesha kwa njia ya mtandao. Tutakuwa tunakutumia kila kipengele kwenye email yako. Kama bado hujajiunga na mtandao huu JIUNGE SASA ili usipitwe na mambo mazuri haya
Malengo ni nini?
Malengo ni shabaha ya namna mtu ataitimiliza kazi yake hapa duniani. Ni mapitio (njia na mbinu) anazopitia mtu hadi akipate kile kikubwa anachokitamani, kwahiyo ndani ya malengo kuna mikakati kadhaa ambayo mtu huiweka ikiwa ni pamoja na kujipa uhuru wa kufanya jambo fulani au kujinyima uhuru au kujizuia kufanya mambo fulani ili akipate kile kikubwa anachokitamani.
Maisha ni safari ndefu yenye vituo vingi pia yenye changamoto nyingi. Tunahitaji kuweka malengo ili tufike tunakotaka kufika vinginevyo hatutafika kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukata tamaa na mambo mengine.
Tunazo sababu kadhaa zinazotufanya tuwe na malengo yetu, sababu hizo ni hizi zifuatazo;-
a) Tujidhibiti katika mienendo yetu, au kwa lugha rahisi tujizuie kufanya baadhi ya mambo yanayoweza kututoa kwenye mstari wa matamanio yetu.
Kuna msemo usemao; “mtu bila maono (Malengo) hushindwa kujizuia”. Msemo huu ni kweli kabisa kama huna ndoto ya kufika mbali kujizuia kwenye baadhi ya mambo yenye uwezo wa kukutoa kwenye mstari wa mafanikio huwa ni vigumu. Jizoeze kuandaa malengo yako tena uyaandike na uyatii utashangaa kuona kumbe kila jambo linawezekana.
b) Akili hushindwa kufikiri ipasavyo ikiwa haijaelekezwa kufikiri kwenye kitu fulani badala yake huona uvivu na kukata tamaa. Lakini kama kuna malengo yalioandaliwa vizuri, akili hupata nguvu zaidi za kufikiri juu ya malengo hayo na hivyo kila siku kupata wazo jipya la kuyafikia malengo yako.
c) Malengo ni picha ya mafanikio yako unayoyaona wakati ukiwa mwanzoni mwa safari ya mafanikio yako. Kama utakuwa unajiona mwenyewe jinsi utakavyokuwa miaka kadhaa inayokuja, itakutia hamasa ya kukazana zaidi ili uifikie hiyo ndoto yako.
d) Sisi binadamu si wa kudumu, leo upo na kesho haupo. Tunahitaji kuweka malengo ya familia zetu ili hata kama wewe hutakuwepo anayebaki asihangaike cha kufanya. Atapitia kwenye malengo uliyoyaacha na akiwa jasiri anaweza kufika kwenye mafanikio uliyoya tazamia. Ndivyo wanavyofanya wenzetu katika nchi zilizoendelea. Utakuta hadi wajukuu wanapitia malengo ya babu yao na wanazidi kufanikiwa zaidi. Tuache tabia ya kujiangalia sisi tu tuangalie na vizazi vyetu kwa kuandaa malengo.
e) Kuweka malengo yako binafsi na familia yako, unawapa somo zuri watoto wako nao watajifunza kupitia wewe na wao wataweka malengo yao yatakayo wasaidia katika maisha yao.
Kumbuka: Malengo ni kipimo kinachotumika kukujulisha umepiga hatua kiasi gani kwenye mafanikio yako. Kama hujaweka malengo yaliyodhahiri sio rahisi kujua kama kuna matumaini ya kufikia ndoto zako. Kwa lugha nyingine usipokuwa na malengo dhahiri (na yaliyoandikwa) unaweza ukachelewa kufikia mafanikio yako au unaweza usifike kabisa maana huna mahali pa kujiangalia. Ndio maana nasisitiza ni muhimu malengo yako uyaandike.
Pamoja na kujiwekea malengo yako kuna jambo moja baya zaidi litakalokuzuia kuyatekeleza malengo hayo;
Soma makala hii ulifahamu: Jambo Moja Kubwa Linalokufanya Ushindwe Kufanya Mambo Unayotaka Kufanya KamaHautalidhibiti Kufanikiwa Usahau.
Nazidi kukumbusha kama bado hujajiunga na mtandao huu bonyeza maadishi haya ili ujue faida sita utakazopata kwa kujiunga na mtandao huu. Pia kwa kujiunga na mtandao huu utakuwa umejisajiri moja kwa moja kutumiwa semina ya kuweka malengo yako kuanzia miaka 20 hadi uzeeni yaani zaidi ya miaka 60.
“Chakushangaza watu wengi sijui kama wewe ndugu ni miongoni mwao, unataka kupata mafanikio bila kuweka mikakati thabiti itakayokupelekea kufikia hayo matamanio yako yaani hujaweka malengo yako au kama yapo hujayawekea utaratibu kama wafanyavyo ndege wa angani. Mimi nakushauri pata nafasi uwatembelee ndege ukajifunze kwao somo hili”.
0 comments :
Post a Comment