Friday, July 7, 2017

TAARIFA YA UTENDAJI KAZI KATIKA SERIKALI YA WANACHUO (ARISO) MWAKA 2016/2017
Tunapenda kumshukuru Mungu wetu kwa wema na ulinzi wake tangu tulipokabidhiwa uongozi hadi leo tuko salaama, jina lake litukuzwe sana.
      Tulikabidhiwa uongizi rasmi tarehe 15/06/2016 na tukiwa  jumla ya wanachuo 171  

Malengo na madhumuni ya taarifa hii ni kujua mafanikio,malengo na changamoto katika serikali yetu ya ariso.

Chama cha ariso kilikuwa na malengo mbalimbali kama yalivyokuwa yanapendekezwa kwenye vikao na kwa kujinadi kipindi tunaomba kura kwenu kama ifuatavyo;


MALENGO
      I.            Kuinua uchumi wa ariso kwa kubuni miradi mbalimali.kama vile kuwa na jiko la kuchoma chipsi , kuwa na photocopy mashine kuwa na mashine ya kutengeneza vitambulisho itakayo kuwa ikitengeneza vitamburisho na vyeti katika chuo chetu na katika vyuo mbalimali na tasisi mbalimbali itakayo kuwa kama kitega uchumi wa ariso.
   II.            Kutengenza brogspot itakayo tumiwa na wanachuo na watu mbalimbali kupata tarifa za chuo.
III.            Kununua computer itakayotunza kumbukumbu za ariso kwa kila mwaka
IV.            Kusimamia matatizo yote ya wanachuo na kuhakikisha kila mwanachuo ameyafikia malengo yake kwa dhati .
  V.            Kusimamia ratiba ya masomo kuhakikisha kila darasa lina pata siku moja kwa kila wiki kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
VI.            Kusimamia swala la maji, chakula pamojan na mazingira kwa ujumla
VII.            Kusimamia pesa na  mali za ariso  

MAFANIKIO;
Mafanikio yaliyopatikana tangu tupewe uongozi ni  mengi , kwa kuyataja kwa ufupi tu.
      I.            Tumefanikiwa kusimamia  matatizo na kero nyingi zinazotukabiri wanachuo kama vile ukosefu wan ndoo, mifagio ya vyumbani taa katika mabweni, taa madarasani, ubovu wa ofisi ya ARISO na mbao za kufundishia na kero zinginezo nyingi.
   II.            Tumefanikiwa kufungua blonspot inayoitwa  arisoardhi.blogspot ambayo ina email. Ariso.ardhi@gmai.com hii itatusaidia wanachuo  kupata habari mbali mabali katiaka chuo chetu.
III.            Tumefanikiwa kupeleka namba za simu za wanachuo na kusajiliwa na vifurushi vya university offer  tigo na voda
IV.            Tumefanikiwa kusimamia swala la ratiba na kuhakikisha kila darasa limepata siku moja kwa kila wiki kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
  V.            Tumefanikiwa kuanzisha mafunzo ya programs zinazoendana na masomo yetu tuliyoyaedesha kwa ratiba za usiku  hii imesaidia kujua program vizuri kwa kila mwanachuo kama vile Autocard na Arc GIS.
VI.            Tumefanikiwa kupewa week moja kwa ajili ya kujifunza practical kwa vifaa vya kisasa ikiwa kama study tua kwa wanafunzi.
VII.            Tumefanikiwa kusimamia swala la maji kwa kuhakikisha maji yanapatikana kwa kila mda na kuomba kuongezewa kwa tank za maji hapa chuoni.
VIII.            Tumefanikiwa kusimamia pesa ya ariso kwa kuhakikisha tumepewa kama pesa ya wanachuo
IX.            Tumefanikiwa na kusajiliwa kwa account yetu ya ARISO na BOT
  X.            Tumefanikiwa kufanya sherehe ya kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa kwanza.
XI.            Tumefanikiwa kusimamia DSTV na kuomba chuo watulipie kifurushi cha DSTV .
XII.            Tumefanikiwa kushirikiana na vyuo vingine katika sherehe mbalimbali kimawazo pamoja na michezo.
XIII.            Tumefanikiwa kununu vifaa vya michezo kama vile mipira
XIV.            Tumefanikiwa kupewa mipira miwili na watu wa LAPF na tumeomba jezi pia bado tunasubilia  .
XV.            Pia tumefanikiwa kujumuika na watu wa tigo wakatupa huduma zao na pia tukafanikiwa kuwaomba watuwezeshe vifaa vya michezo kama vile  jezi pamoja na mipira na pia wakakubari kuwashirikisha katika sherehe zozote pale tunapoandaa sherehe zetu kama vile welcome first year na graduation .

CHANGAMOTO
Zifutazo ni changamoto zilizo tukabiri katika utendaji kazi
      I.            Ukosefu wa mtaji utakao tuwezesha kuendesha miradi mbalimbali  itakayo kuwa kama kitega uchumi wa ariso.
   II.            Kutotekelezewa kero zetu mapema pale tunapo pata changamoto hapa chuoni .
III.            Ukosefu wa viwanja vya michezo hili limekuwa likitupa wakati mgumu sana pindi tunapohitaji mazoezi
IV.            Kutokuwa na bima kwa baadhi ya wanachuo hii imekuwa ikitupa wakati mgumu pale mwanachuo anapopatwa na tatizo kama vile kuumwa hadi inapelekea kwa viongozi kutumia pesa zao kutoka mifukoni mwao kumsaidia mwanachuo.
MAPENDEKEZO
·       Tunapendekeza uongozi utakao kuja uhakikishe kusimamia  kero bila kurudi nyuma
·       Mapendekezo yetu kuwa kwa wanachuo wote ambao hawana bima za afya ni ushauri kuwa kila mwanachuo awe na bima ya afya hii itamsaidia pale anapokuwa na tatizo lolote la kiafya .
·       Uongozi ujao usimamie swala la practical kwa kila darasa lipate hata siku moja kwa week.
·       Pia tunapendekeza viongozi watakaochaguliwa wasimamie kujifunza kwa programs na kuhakikisha kila mwanachuo anajua hizo software.
HITIMISHO
Shukrani za pekee kwa wanachama wote wa ariso  kwa ushirikiano wenu katika uongozi wetu muendele na moyo wa kusaidiana ili kuanda maisha yetu kwa pamoja na kuijenga ariso.

kwa niaba ya viongozi wenzangu tunasema asanteni sana Mungu awe pamoja nanyi awaongoze katika maandalizi ya mitihani na katika mitihani yetu.

Tuesday, April 18, 2017

WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO  YA MAKAZI  CHUO CHA ARDHI MOROROGO
RISALA YA  WANAFUNZI WA  CHUO  CHA ARDHI MOROGORO KWA MGENI RASMI MAHAFALI YA 35 YA CHUO CHA ARDHI
TAR 24/03/2017
Ndugu mgeni rasimi,
Awali ya yote tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kufika kwako hapa chuoni ,tunatambua kuwa umeacha shughuli zako nyingi za kiofisi na ukakubali kuchukua muda wako kuja kujumuika nasi katika shughuli ya kuwaanga ndugu zetu kwa pamoja tunasema asante sana Mungu awe pamoja nawe na karibu sana.
Ndugu mgeni rasimi;
Chuo hiki kiko chini ya  wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kilisajiliwa na Baraza la Taifa la elimu ya ufundi Tanzania (NACTE) tangu  tarehe 21/5/2002 na  chuo kinatumia mitaala ambayo ni “Competence based “ chuo kilipata  ithibati kamili (Full Accreditation) ya NACTE tangu mwaka 2010. Baada ya kutimiza vigezo vya elimu na mazingira ya uboreshaji elimu hiyo.


LENGO LA RISALA:
Ndugu Mgeni Rasmi,
Lengo la risala hii ni kukujulisha kuhusu mafanikio, changamoto, maoni na mapendekezo katika kuboresha hali ya kitaaluma na maisha mengine nje ya taaluma Chuoni hapa.

Ndugu mgeni rasimi; Chuo kinatoa kozi ya Jiomatikia katika ngazi zifuatazo:
Cheti cha awali cha Jiomatikia (Basic Certificate in Geomatics (NTA LEVEL 04)),
Astashahada ya Jiomatikia (Certificate in Geomatics (NTA LEVEL 05)),
Stashahada ya Jiomatikia (Diploma in Geomatics (NTA LEVEL 06)).
Ndugu mgeni rasimi:
Katika mahafali ya leo, kuna jumla ya wahitimu 171 kati yao wanafunzi wa jinsia ya kiume wakiwa ni 136 Na jinsia ya kike wakiwa  ni 35.
Ndugu mgeni rasimi;
Mafanikio yaliyopatikana tangu chuo chetu kianzishwe ni mengi , kwa kuyataja kwa ufupi tu ni kwamba kila mwaka chuo kimekuwa  kikizalisha wataalamu wazuri wenye kuleta ufanisi katika taaluma hii ya upimaji Aridhi, nchini ambao wameajiriwa katika Halmashauri mbalimbali na hivyo kuipunguzia serikali utegemezi wa wataalamu wa kigeni katika idara ya upimaji Ardhi.

CHANGAMOTO
Ndugu mgeni rasimi:
Malengo ya serikali ni utekelezaji wa sera ya upimaji ardhi kwa ajili ya mashirika na taasisi mbalimali, kutokana na ukosefu wa ajira wataalamu wengi hawanufaiki na taaluma inayotolewa katika chuo hiki hadi kupelekea wengi wetu kupoteza taaluma zetu kwa kukaa tu bila ajira. ndugu mgeni rasimi:
 kutokana na tatizo la ajira tunaamni wizara yako inao uwezo wa kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hili kwa kutoa ajira pindi tunapomaliza muda wa mafunzo.
Ndugu mgeni rasimi:
Tunalo tatizo katika chuo chetu la kukosa vitendea kazi kwa ajili ya masomo yetu; Tunao Ukosefu wa maktaba (Library) kwani iliyopo bado haijaisha, jengo hili la maktaba limekuwa na muda mrefu tangu lifikie hatua hiyo, kwa sasa tuna  chumba kidogo cha kutunzia vitabu hivyo hali hii inatupa wakati mgumu wa kujisomea kwani tunakosa vitabu vya kutosha.
Ndugu mgeni rasimi;
 Tunao Ukosefu wa chumba cha computer (Computer Lab) kwani kilichopo ni kidogo chenye computer chache na baadhi ni mbovu hazitumiki, pia computer hizi hazina program za kitaaluma (software).
Ndugu mgeni rasimi;
Tunao Upungufu wa vifaa vya kujifunzia vinavyo endana na taaluma yetu kwani vilivyopo ni vichache, na vingine vimeshapitwa na wakati tunaomba tupatiwe vifaa za kisasa kama vile RTK GPS, na Differential GPS za kutosha ili tupate elimu inayoendana na wakati.
Ndugu mgeni rasimi;
Tunao Ukosefu wa vibweta vya kujisomea kwenye mazingira ya chuo, hivyo wanachuo kufanya majadiliano ya kimasomo (Group Discussion) kwenye mazingira magumu,
Ndugu mgeni rasimi;
Serikali kupitia wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi  ilikuwa ikitupatia  stationary Allowance Tsh 50,000 /= kila mwanachuo,  pesa hii ilikuwa inasaidia kumudu gharama zote za stationary kwa wanachuo lakini mwaka wa masomo 2016/2017 hatujapewa hii imepelekea kwa mwanchuo kuto mudu gharama za stationary.
Ndugu mgeni Rasimi;
 ombi letu kuwa serikari kupitia wizara ya Ardhi Nyuma na Maendeleo ya makazi ituhudumie stationary allowance kwa kila mwanafunzi kwa kila mwaka kama ilivyokuwa hapo awali, pia tunaomba mchakato wa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati uharakishe ili kupunguza ugumu wa kugharamia elimu wazazi wetu.
Ndugu mgeni rasim;
Miundombinu mingi imechakaa na ina tufanya tuishi katika mazingra magumu; Uchakavu wa madarasa (madirisha, feni na mifumo ya umeme kusababisha hitilafu kila mara madarasani). Mabweni yaliyopo yamechakaa sana, sakafu, paa, kuta, madirisha, na milango vimechakaa sana kiasi cha kutokuwa rafiki kwa wanachuo na hayatoshi. Hivyo kupelekea kukaa wanafunzi wastani wa sita mpaka nane chumba kimoja. Uchakavu wa vyoo vyote vinavyo patikana hapa chuoni kwani vingi havijafanyiwa ukarabati vinaziba mara kwa mara na kusabisha usumbufu kwa wanachuo.
Ndugu mgeni rasimi;
Chuo hakina viwanja vya michezo, hii inatupa wakati mgumu tunapohitaji mazoezi nakupelekea kushindwa kuendesha michezo hapa  chuoni. Tunaomba uwezeshwaji kutoka wizara yako wa kujenga eneo la chuo lililopo mlima kola. Tunao upungufu wa tank za kutunzia maji, hii imepelekea kutokuwa na uhakika wa maji hapa chuoni kwani tank iliyopo ni ndogo na halikidhi mahitaji.




Ndugu mgeni rasimi;
tunakutakia kila la kheri katika kazi zako za ujenzi wa Taifa na tunatumaini na kuamini  kuwa matatatizo tuliyowasilisha kwako katika risala hii yatapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Nasi kwa pamoja tunashukuru sana kwa kuweza kuonesha moyo wa upendo, kujali na kuvumilia yote na kuweza kufika hapa chuoni isiwe kikomo chako cha kututembelea mara kwa mara kujua maendeleo ya chuo chetu na mapungufu yatakayojitokeza katika chuo chetu tukiwa kama wanafamilia wa wizara yako Mungu awe pamoja nawe .

Risala hii imeandaliwa na Mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Ardhi Morogoro
NDG. MAGOMBA  PETER  MAHOTA- RAIS ARISO

………….Ahsante sana…………..



Thursday, March 23, 2017

MAHAFALI YA 35 YA CHUO CHA ARDHI MOROGORO 

Ndugu wanachuo wote mnajulishwa kuwa mahafali ya kuwaanga wahitimu wa masomo ya  stashahada ya Jiomatikia (Diploma in Geomatics) wa mwaka wa masomo 2015/2016 yatafanyika tarehe 24/03/2017 unakaribishwa kujionea mwenyewe ndugu mgeni rasimi Kaimu katibu mkuu wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi akiwatunuku vyeti wahitimu wa masomo ya 

Cheti cha awali cha Jiomatikia (Basic Certificate in Geomatics (NTA LEVEL 04)),wa mwaka wa masomo 2015/2016
Astashahada ya Jiomatikia (Certificate in Geomatics (NTA LEVEL 05)),wa mwaka wa masomo 2015/2016
Stashahada ya Jiomatikia (Diploma in Geomatics (NTA LEVEL 06)).wa mwaka wa masomo 2015/2016

Thursday, November 3, 2016


TIME TABLE FOR DEMONSTRATION OF GEOMATIC PROGRAMS-ARIMO 2016-2017  

Special Software:-

  •  AutoCAD Land Development.
  •   Arc Map& Google Earth.
  •  Cad pro &Csco3.
  •  AutoCAD Civil Design.
S/N
PROGRAM
SPECIFIC HINTS
TIME USE
1
AutoCAD Land Development
Introduction of AutoCAD







3  Days
How to open project
How to input data(coordinates)in AutoCAD
How to draw Cadastral survey plan with
  •   To calculate area
  • To calculate Distance
  •   To insert Grids
  •   To drawn cadastral plan frame
  •  To print Cadastral plan
How to geo referencing TP drawing with
  •   Inquiring Coordinates
  •  Prepare Cadastral plan from TP drawing.

How to prepare Deed plan.
2
Arc Map & Google Earth













Introduction of Arc Map









3 Days
How to open project

How to input data
  •  Image 
  •  Coordinate

How to prepare Thematic Map

  • Geo referencing of Topo sheet
  •  Digitization of Features
  •   Prepare Frame of Thematic map
  •  Printing Thematic Map
Introduction of Google Earth
  •  Input data from Arc map
  •  Export data from Arc Map
  • Import data to Arc Map
How to digitized in Google Earth

How to prepare locality sketch

3
Cad pro &Csco3.

Introduction of Cad pro & Csco3






3 Days


How to input datum




How to compute with Cad pro & Csco3
  •  Traverse
  • B&D
  •  On line
  • Area
  •  Road with check
  • Join comps(Check Distance)


How to make Transformation
  •  TTM-UTM
  • UTM-TTM
4
AutoCAD Civil Design.& Excel in Designing

Introduction




3 Days
How to input data
How to draw contours
How to draw Longitudinal Profile
How to draw  Cross section
How to design the Drainage system in Excel.


  1. DEMOSTRACTORS
  2.   PETER MAGOMBA-NTA LEVEL 6 
  3.   PETER EMANUEL-NTA LEVEL 5
  4.   HUSSEN DUMA-NTA LEVEL 6
  5.   MAKOYE WEBIRO-NTA LEVEL 6
  6.   GOODLUCK KILONGOZI –NTA LEVEL 6
  7.     AND OTHERS


THE END